Header Ads

Header ADS

Collabo zamiminina kwa Vanessa Mdee ameshirikishwa na msanii Malawi, Togo na mwingine wa Ufaransa

Vanessa Mdee ni hot cake kwa sasa barani Afrika.                                                                                                       Wasanii kibao wanataka wamshirikishe, na wengine ni kutoka kwenye nchi ambazo ni ngumu kwa msanii wa Tanzania kuzipata. Moja ya nyimbo alizoshirikishwa ni ya msanii wa Ufaransa, Lylah na tayari video ya wimbo wao imeshafanyika.13257024_118322398586338_1901852589_nVanessa akiwa na msanii wa Ufaransa, Lylah
“Lylah ni msanii ambaye amekuwa akijaribu kuingia kwenye African market, anaimba Kifaransa na Kiingereza. So walifanya research they reached our team na nilivyokuwa Nigeria wakaja, wakapanga vitu vyote tukamalizia Nigeria,” 
Pia Vee Money amedai ameshirikishwa na kundi kubwa la muziki la nchini Togo.
Anadai kuwa wimbo huo utampa nafasi ya kuimba muziki kwa Kifaransa, lugha ambayo anaijua vyema.
Hivi karibuni pia Vanessa aliingia studio kurekodi wimbo alioshirikishwa na msanii wa Malawi, Tay Grin                   .13573390_721625491313757_865502197_nVanessa na Tay Grin
Bado ana collabo na Patoranking, Tekno na wasanii wengine wakubwa Afrika.

No comments

Powered by Blogger.