Chris Smalling aanguka ghafla kwa kula chakula ambacho kina sumu
Beki wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa England Chris Smalling ameumia vibaya kwa kupasuka juu ya jicho baada ya kuanguka ghafla na kujigonga akiwa katika mapumziko katika kisiwa cha Bali nchini Indonesia.
Jeraha lake limeelezwa kuwa na ukubwa wa inchi tatu na kulazimika kushonwa nyuzi kadhaa
Inaelezwa Smalling alianguka baada ya kula chakula chenye chembechembe ambazo huenda kuwa zinatokana na samaki au mbogamboga ambazo si zile zinazowekwa kwa makusudi.
Smalling alikuwa na mpenzi wake Sam Cooke na alianguka na kupelekwa hospitali kupatiwa matibabu na anaendelea vizuri.
No comments