Header Ads

Header ADS

Afande Sele amfuta machozi Nay wa Mitego

Msanii wa muziki wa Hip Hop kutoka Morogoro, Afande Sele amempa pole rapper mwenzake Nay wa Mitego ikiwa ni siku moja toka Baraza la Sanaa la Taifa limfungie rapper huyo kwa muda usiojulikana baada ya kukutwa na makosa matatu                                                                                                                     .Aidha, rapper huyo ametakiwa kulipa faini ya shilingi milioni 1 pamoja na kuwaomba msamaha mashabiki wa muziki wake.
Afande ameonyesha kutopendezwa na adhabu hiyo huku akidai kuna wasanii wengi wanafanya vitendo kama vya Nay wa Mitego lakini hawachukuliwi hatua.
“Sio jambo lakuchukiza likini linafadhaisha pale unapojiuliza kwani aadhibiwe yeye tu?,” Afande aliuliza kupitia instagram yake.
Aliongeza, “Mbona kuna wenzake wengi tu walifanya na wanaendelea kufanya makosa kama yake au zaid lakini hawajachukuliwa hatua kama yeye?. Ni Siasa, mapenzi, undugu au, pole askari wangu mdogo mpiganaji stadi yatakwisha tu, tutawasimulia kina Shishi Baby, Snusex na wengine kuwa ‘hainaga ushemeji’,”

No comments

Powered by Blogger.