TIZAMA;Serikali yaitaja mikoa 5 masikini zaidi Tanzania
Serikali imesema Kigoma, Geita, Kagera, Mwanza pamoja ni Singida ndiyo mikoa masikini zaidi Tanzania huku Dar es salaam, Kilimanjaro, Pwani, Arusha na Manyara ikiwa ni mikoa mitano yenye ahueni ya umasikini nWaziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, alisema hayo jana wakati akiwasilisha bungeni mjini hapa taarifa ya hali ya uchumi ya mwaka 2015 na mpango wa maendeleo wa taifa kwa mwaka wa fedha 2016/17.
Alisema tathmini ya hali ya umaskini kimaeneo iliyofanyika kwa kutumia takwimu za sensa ya watu ya mwaka 2012 na utafiti wa hali ya kipato na matumizi katika kaya wa mwaka 2012, unaonyesha matokeo chanya na kutofautiana kimkoa na wilaya.
Dk. Mpango alisema mkoa wa Kigoma unaongoza kwa kuwa na umaskini mkubwa wa asilimia 48.9, ukifuatwa na Geita (asilimia 43.7), Kagera (asilimia 39.3), Singida (asilimia 38.2) na Mwanza (asilimia 35.3).
Pia Waziri huyo alizitaja wilaya maskini zaidi nchini kuwa ni Kakonko (Kigoma) na Biharamulo (Kagera) ambazo asilimia 60 ya watu wake wapo chini ya mstari wa umaskini wa mahitaji ya msingi.
“Hii ina maana kuwa maeneo ya vijijini, hususan pembezoni bado watanzania wengi wanaishi kwenye umaskini na uwezo wao wa kupata mahitaji ya msingi ni mdogo,” alisema.
Dk. Mpango aliendelea kueleza kuwa, mkoa wa Dar es Salaam unaongoza kwa kuwa na ahueni ya asilimia 5.2 ya umaskini wa kipato, ukifuatia Kilimanjaro na Pwani (yote asilimia 14.7) na Manyara (asilimia 18.3).
Hata hivyo, Waziri huyo alisema pato la wastani la Mtanzania limekua kutoka Sh. 770,464 mwaka 2010, hadi Sh. 1,918,928 mwaka 2015.chini
No comments