Header Ads

Header ADS

TIZAMA;Queen Darleen asema alikuwa mfanyakazi ndani ya ‘WCB’ kabla ya kusaini kama msanii

Msanii wa muziki ambaye pia ni dada wa staa wa muziki Diamond Platnumz, Queen Darleen baada ya kusaini WCB hivi karibuni, amefunguka na kueleza jinsi alivyokuwa ananufaika na mafanikio ya kaka yake.Akizungumza  Jumatatu hii, Queen Darleen amesema alikuwa ni mfanyakazi wa kawaida ndani ya WCB na alikuwa akilipwa mshahara kama wafanyakazi wengine.
“Kabla ya kusaini WCB maisha yangu yalikuwa yameshabadilika,” alisema Darleen “CEO tayari alikuwa ameshanibadilishia maisha yangu, nilikuwa nafanya kazi mbalimbali ndani ya WCB na nilikuwa nalipwa, kama zile behind the scenes nilikuwa nazisimamia mimi,”
Muimbaji huyo amezungumzia hatua ya kusaini ‘WCB’.
“WCB ni label ambayo inafanya poa kwa sasa, kwa hiyo kufanya kazi chini ya ‘WCB’ ina maana kwamba muziki wangu sasa unaenda katika level nyingine, hii ni hatua nzuri, tuombe Mungu mambo yaende vizuri, muziki wangu utafika mbali zaidi, kwa hiyo mashabiki wakae mkao wa kula kwa ajili ya vitu vipya na vizuri, nini ndiye Queen ‘WCB’,” alisema Darleen.

No comments

Powered by Blogger.