Header Ads

Header ADS

Sh1.5 bilioni za Umiseta na Umitashumta zapelekwa kwenye madawati

Wakati Tanzania ilikiendelea kusuasua katika michezo, serikali imesema zaidi ya Sh1.5 bilioni zilizotakiwa kutumika kwa ajili ya fainali za michuano ya wanafunzi wa shule za msingi (Umiseta) na Sekondari (Umitashumta) zitaelekezwa kwenye utengenezaji wa madawati, baada ya michuano hiyo kusimamishwa.????????????????????????????????????
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene alisimamisha michuano hiyo ili kufanikisha agizo la Rais John Magufuli la kuhakikisha hakuna mwanafunzi atakayekaa chini ifikapo Juni 30
Akizungumza baada ya mdahalo kuhusu namna ya kuimarisha uhusiano baina ya wawekezaji na wananchi ulioandaliwa na Taasisi ya Uongozi, jijini Dar es Salaam, Simbachawene amesema hakutakuwa na maana kama fedha nyingi zitatumika kwenye michezo wakati wanafunzi wanakaa chini.
“Kama michezo wameshacheza na walikuwa wanaelekea Taifa, hatujazuia isipokuwa tumesimamisha hadi pale tatizo la madawati litakapoisha,”amesema.

No comments

Powered by Blogger.