Header Ads

Header ADS

Ronald Koeman awa meneja mpya wa klabu ya Everton

Klabu ya Everton imethibitisha usajili wa kocha Ronald Koeman kuwa meneja wao mpya kwa mkataba wa miaka mitatu.
Everton wametoa dola milioni 5 kama fidia kwa kocha huyo mwenye miaka 53 ambaye anaihama klabu ya Southampton baada ya kuisimamia kwa miaka miwili.
Everton ilikuwa bila kocha tangu ilipomtimua Roberto Martinez kabla ya mwisho wa msimu uliopita.
Koeman amesema kuwa Everton ni klabu yenye historia kubwa na ari ya kutaka kushinda huku mwenyekiti wa klabu hiyo akimwita raia huyo wa Uholanzi kama lengo lake la kwanza.
35412EBA00000578-3640463-Everton_tweeted_this_picture_after_confirming_Ronald_Koeman_as_t-a-1_1465895828068

No comments

Powered by Blogger.