Header Ads

Header ADS

Jamie Vardy akubali kusaini mkataba mpya na Leicester

Mshambuliaji wa klabu ya Leicester na Uingereza Jamie Vardy hatimaye amekubali kusain mkataba mpya na Leicester.jamie_vardy_leicester_city_wallpaper_by_fbwallpapershd-d9vapjvLeicester imesema kuwa mchezaji huyo mwenye miaka 29 ambaye ali isaidia klabu yake kushinda taji la ligi ya Uingereza msimu uliopita ameongeza mkataba wa miaka minne na klabu hiyo.
”Pande zote mbili zinatumai tangazo hilo litamaliza uvumi wa hivi karibuni kuhusu hatma ya Jamie”,taarifa ya klabu imesema.
Vardy alitarajiwa kununuliwa na klabu ya Arsenal kwa kitita cha pauni milioni 20 na Arsenal kabla ya kuanza kwa michuano ya Euro 2016 huku The Gunner ikitoa kitita cha pauni 120,000 kila wiki kwa mchezaji huyo.
Leicester nayo ilijibu kwa kutaka kumpatia pauni 100,000 kwa wiki.

No comments

Powered by Blogger.