Header Ads

Header ADS

Darassa asema hili, baada ya Linah kusema anatamani kuzaa na mwanaume mwenye sifa kama zake

Baada ya mwanadada Linah Sanga kusema anatamani kuzaa na mwanaume mwenye sifa kama za Darassa, rapa huyo wa wimbo ‘Kama Utanipenda’ amefunguka na kuzungumzia kauli hiyo.
Akiongea  Jumanne hii, Darassa amesema anaheshimu mawazo ya mwanadada huyo.
“Hiyo ni kauli yake, naheshimu mawazo yake. Nimefunzwa kuheshimu maoni ya kila mtu, kwa hiyo sina la kuzungumza zaidi ya hapo kwa sababu hizo ni issue za privacy za watu,” alisema Darassa.
Katika hatua nyingine Darassa amewataka mashabiki wake wa muziki kukaa mkao wa kula wa ujio wa kazi yake mpya ambayo ataiachia katikati ya mwezi huu.
11950746_1506685152991715_1450290419_n

No comments

Powered by Blogger.