Header Ads

Header ADS

Ben Pol afungua mlango kwa label inayotaka kumsaini

Mkali wa wimbo ‘Moyo Mashine’ Ben Pol amesema kwa sasa yupo tayari kusaini kwenye label yeyote ambayo itakuwa na nia ya kumpeleka mbali zaidi kimuziki.Ben-Pol-2
Akiongea  wiki hii, Ben Pol amesema label ambayo anahitaji ni ile ambayo itamtoa alipo sasa na kumpeleka katika level nyingine.
“Mimi sasa hivi nakaribisha proposal za management, kama management au label inataka kufanya kazi na Ben Pol iniambie itanifanyia kitu gani, kwa sababu kama kampuni sasa hivi inakuja inaniambia itapeleka nyimbo zangu MTV au wapi sasa hivi mimi nyimbo zangu zinachezwa huko na nilipeleka mwenyewe, hiyo management hainifai kwa sababu hivyo nimeshafanya mwenyewe. Management ikinionyesha kitu ambacho siwezi kufanya kwa sasa tunaweza fanyakazi,”
Bep Pol alisema kwa sasa hana management lakini ana watu ambao anafanya nao kazi kwa ukaribu zaidi ambao pia humshauri mambo mbalimbali kuhusu muziki wake

No comments

Powered by Blogger.