Aliyemuua staa wa US Christina Grimmie alikuwa shabiki aliyekuwa akimpenda kupitiliza
Kifo cha staa wa Marekani aliyejipatia umaarufu kupitia shindano la The
Voice Christina Grimmie hivi karibuni kimewasikitisha mastaa na watu
wengine.Na sasa imebainika kuwa aliyemuua muimbaji huyo alikuwa shabiki wake aliyempenda kupitiliza.
Muuaji huyo alijaribu kufanya kila awezalo ikiwemo kujibadilisha muonekano wake ili tu Christina amuone na iliposhindikana aliamua kumuua. Wafanyakazi wenzake na Kevin Loibl wameiambia TMZ kuwa alimpenda Christina hadi kuamua kupandikizwa nywele mpya na kufanyiwa upasuaji wa macho.
Pia aliamua kutotumia nyama na bidhaa zake ili kupunguza uzito. Wanasema alikuwa akisikiliza muziki wake kazini na kuapa kuwa lazima muimbaji huyo angekuja kuwa mke wake.
Pia inasemekana kuwa taarifa kuwa Christina alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na producer wake zilimkasirisha. Hasira hiyo ilimfanya aende kwenye show yake Ijumaa iliyopita na akampiga risasi ya kichwa na kisha kujiua pia.

No comments